TAASISI zinazohudumia mahujaji Zanzibar (UTAHIZA) zinakusudia kuandaa muongozo wa pamoja kuanzia maandalizi hadi safari za hija ili kuondoa usumbufu kwa mahujaji. Continue reading “UTAHIZA KUANDAA MUONGOZO WA HIJA WA PAMOJA”
WAISLAM MSITOE FATWA BILA YA ELIMU – SHEIKH OMAR BIN HAFIDH
WAUMINI wa dini ya Kiislam wametahadharishwa kutoa maamuzi ya usuluhishi wa masuala ya dini yao bila ya kuwa na elimu ya uelewa wa mambo ya dini ambayo msingi wake umejengwa na wanazuoni waliopita.
Continue reading “WAISLAM MSITOE FATWA BILA YA ELIMU – SHEIKH OMAR BIN HAFIDH”
Wazazi watakiwa kuwafuatilia watoto wao
WAZAZI wametakiwa kufuatilia maendeleo ya watoto wao katika vyuo na kwengineko na kuachana na tabia ya kuwaachia walimu pekee ili kurahisisha mafunzo ya watoto wao. Continue reading “Wazazi watakiwa kuwafuatilia watoto wao”
Waislam someni elimu ya ndoa – Abdulrahman Bakar Muhana
Wanawake wa kiislamu nchini wametakiwa kuipa kipaumbele zaidi elimu ya ndoa ili kuepusha kuvunjika kwa ndoa zao.
Continue reading “Waislam someni elimu ya ndoa – Abdulrahman Bakar Muhana”
Waislam watakiwa kuifanyia kazi Qur’an
Waislam nchini wametakiwa kuisoma Qur’an na kuifanyia kazi ili iweze kuwasaidia katika maishayaoya kila siku. Continue reading “Waislam watakiwa kuifanyia kazi Qur’an”
WANASIASA WAACHE MZAHA NA QUR’AN-BARAZA LA WANAWAKE WA KIISLAM
Msimamizi Mkuu wa Baraza la Wanawake wa Kiislamu Tanzania Sheikh Abdalla Abass Mnubi ameiomba ofisi ya Mufti Zanzibar kupiga marufuku kusomwa Qur’an katika mikutano ya kampeni za vyama vya siasa kwani kufanya hivyo ni kukishushia hadhi kitabu hicho kitukufu. Continue reading “WANASIASA WAACHE MZAHA NA QUR’AN-BARAZA LA WANAWAKE WA KIISLAM”
WANAWAKE WA KIISLAM WATAKIWA KUSOMA KWA BIDII
Wanawake wa Kiislam Zanzibar wametakiwa kuamka kwa kusoma kwa bidii na kuwasomesha watoto wao elimu ya dini ya Kiislam pamoja na kuwahifadhisha Qur-an ili waweze kuondokana na matatizo mbali mbali katika maisha yao.
Continue reading “WANAWAKE WA KIISLAM WATAKIWA KUSOMA KWA BIDII”
Waislam watakiwa kuachana na vyombo vya habari vinavyochochea zinaa.
Waislam wametakiwa kujiepusha na vyombo vya habari vinavyochangia kuenea kwa zinaa.
Hayo yamesemwa katika Ukhty Ramla Abdulrahman alipokuwa akitoa mada juu ya zinaa na madhara yake katika shura ya walimu wanawake wa madrasa za Qur-an iliyofanyika Disemba 5 katika ukumbi wa Al Madrasat Falaah Kijangwani. Continue reading “Waislam watakiwa kuachana na vyombo vya habari vinavyochochea zinaa.”
“Vijana zidisheni mapenzi kwa Mola wenu” UKUEM
Vijana wametakiwa kuzidisha mapenzi kwa mola wao kwa kufuata maamrisho ya dini yao na kuacha makatazo.
Hayo ameyasema Mjumbe wa Kamati ya Uongozi wa Jumuiya ya Umoja wa Kiislam Uchumi Elimu na Maendeleo Wanawake Ukhty Fatma Salim Saleh alipokuwa akifunga semina ya siku tano ya mafunzo ya Kiislam kwa wanafunzi wanawake waliomaliza kidatu cha nne huko katika Chuo cha Wanawake cha Malezi ya Kiislam Muslim Women Academy (MUWA) yaliyofanyika Novemba 7 Chukwani. Continue reading ““Vijana zidisheni mapenzi kwa Mola wenu” UKUEM”
Wanawake wa Kiislam watakiwa kuutumia afya zao kwa ajili ya Allah
Waislam wametakiwa kuzitumia vizuri afya zao wakiwa wazima kwa kukithirisha kufanya ibada kabla hayajawafikia mauti au maradhi.
Wito huo umetolewa na Ukhty Mwanaate Juma alipokuwa akiwasilisha mada juu ya Jichumie mambo matano kabla ya matano katika Shura ya walimu wanawake wa madrasa za Qur-an iliyofanyika Novemba 7 huko katika ukumbi wa Al Madrasat Falaah Kijangwani. Continue reading “Wanawake wa Kiislam watakiwa kuutumia afya zao kwa ajili ya Allah”